Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa BMT, Henry Lihaya amesema, Sekta ya michezo ni muhimu sana katika maendeleo na makuzi ya vijana pamoja na kuhakikisha vijana hawapotei katika umri ambao wanaweza kufanya mambo yasiyiostahili katika jamii.
Lihaya amesema, vijana wanatakiwa kuelekezwa katika michezo ili waweze kuondokana na vitendo ambavyo vinaweza kuwaharibia maisha yao ya baadaye.
Lihaya amesema, kama jamii na Serikali itajitokeza kusaidia katika michezo, itakuwa imesaidia kwa upande wa vijana ambao watakuwa na nafasi kubwa ya kushiriki katika michezo na kuachana na mambo yasiyo na faida kwa jamii.
Lihaya amesema, licha ya kusaidia vijana hao, jambo kubwa na la kufanya ni kuweza kusaidia kulinda viwanja ambavyo huchukuliwa na kutumiwa tofauti na ilivyopangwa hivyo kufanya vijana kushindwa kushiriki michezo mbalimbali kutokana na kukosa viwanja.