Akitoa taarifa kumuhusu, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally amesema kocha Benchikha amerejea kwao kwa lengo la kusoma na atarejea nchini baada ya masomo.
Ahmed amesema kocha msaidizi wa timu hiyo Farid Zemiti kwa kushirikiana na Selemani Matola watakiongoza kikosi hicho hadi pale atakaporejea Benchikha ambaye ataikosa michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Machi 9, 2024 na dhidi ya Singida Fountain Gate utakaochezwa Machi 12, 2024