Kocha mpya wa Argentina, Edgardo Bauza.
Kocha huyu anachukua nafasi iliyoachwa na Gerardo "Tata" Martino aliyejiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Copa America.
Chama hicho kilimtangaza kocha huyo baada ya klabu ya Sao Paulo kukubali kumuachia kocha huyo kwenda kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina.
Bauza, mwenye umri wa miaka 58, alikua kocha mkuu wa klabu ya Sau Paulo toka mwaka 2015 na kuisaidia kufika nusu fainali ya michuano ya Copa Libertadores.
Aidha, kocha huyo ataiongoza Argentina katika kufuzu Kombe la Dunia mwezi Septemba na atamkosa mshambuliaji Lionel Messi kufuatia kustaafu kwake soka la kimataifa.








