![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/09/26/WhatsApp Image 2023-09-26 at 5.44.45 PM.jpeg?itok=gF-p8QbK×tamp=1695740185)
Frank De Jong anakosekana kwenye mchezo wa leo kutokana na kuumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa Ligi Kuu siku ya Jumapili dhidi ya Celta Vigo mchezo ambao Barcelona ilishinda kwa mabao 3-2. Inaripotiwa kuwa De Jong atakuwa nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi November.
Mchezaji mwingine mwenye majeruhi atakayekosekana ni kiungo raia wa Hispania Pedri mwenye majeruhi ya muda mrefu na inatarajiwa atarejea katika ya mwezi Oktaba. Hakuna mchezaji mwingine wa Barcelona aliyeripotiwa kuwa na majeraha na kocha Xavi Hernandez ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakuwa sehemu ya mchezo wa leo dhidi ya Mallorca. Mchezo huu utachezwa Saa 4:30 Usiku.