
Beka amesajiliwa Sports iliyopanda tena ligi kuu ya soka Tanzania Bara kutoka Fanja FC ya Oman aliyoichezea kwa msimu uliopita.
Katika taarifa yake, Beka amesema, amechagua kusaini Sports kwa sababu Tanga ni nyumbani kwao na anaamini huko atapata nafasi ya kucheza na kukuza kiwango chake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, alitua Yanga SC mwaka 2013, akitokea Coastal Union ya Tanga pia, ambayo ilimpandisha kutoka timu yake ya vijana.