
Mchezo wa Arsenal na Huddersfield
Arsenal na Huddersfield jumla zimekutana mara mbili katika EPL tangu Huddersfield ilipopanda katika ligi hiyo mwaka 2016, ambapo Arsenal imefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yote kwa jumla ya idadi ya mabao 7 huku Huddersfield ikiambulia bao moja pekee.
Mpaka sasa, Arsenal imecheza michezo 15, ambapo imeshinda jumla ya michezo 9, ikipoteza mechi mbili na kutoka sare mechi 4. Kwa upande wa Huddersfield yenyewe katika michezo 15, imeshinda mechi mbili, sare nne na kupoteza mechi 9.
Mchezo uliopita, Huddersfield imepoteza ugenini dhidi ya AFC Bournemouth kwa mabao 2-1 huku Arsenal ikitoka sare ya mabao 2-2 na Manchester United.
Kumbuka kuwa mchezo huu utakuwa 'live' kesho Jumamosi kuanzia saa 11:30 jioni kupitia EATV na TV1, Usikose kutazama.