Jumatatu , 23rd Jan , 2017

Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC leo wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuichapa Cosmopolitan ya ligi daraja la pili mabao 3-1 katika mchezo wa raundi ya tano uliopigwa katika dimba la Azam Complex

Wachezaji wa Azam

Kwa hatua hiyo, Azam inaungana na washindani wao wa karibu katika soka la Bongo, Simba na Yanga ambazo nazo tayari zimeshafuzu hatua hiyo kupitia mechi zao za mwishoni mwa wiki.

Katika mchezo wa leo Azam walibanwa kikamilifu katika kipindi cha kwanza na kushindwa kupata bao lolote, lakini katika kipindi cha pili waliongeza mashambulizi na kuweza kupata mabao hayo matatu.

Furaha ya mabao ilianza dakika ya 69 kupitia kwa nahodha John Bocco aliyewahi mpira ulikuwa ukitaka kupigwa na golikipa, mpira ambao ulimgonga Bocco na kuingia wavuni kiulaini kabisa.

Mabao mengine yamefungwa na Shaaban dakika ya 76 na Joseph Mahundi dakika ya 80 huku Cosmopolitan wakipata bao dakika ya 78.

Mara baada ya mchezo huo, nahodha John Bocco ameshukuru kwa kupata ushindi huku akiipongeza Cosmo kwa kuonesha ushindani hasa katika kipindi cha kwanza.

Kuhusu kushangilia, Bocco amesema kutokana na ukweli kuwa hiyo ni timu ambako ametoka kabla ya kujiunga na Azam, aliahidi kutoshangilia, hivyo hata alipofunga bao la kwanza hakushangilia na pia katika bao la pili ambapo yeye ndiye aliyetoa pasi ya bao, hakutaka kushangilia pamoja na wenzake.

Katika mchezo mwingine Stand UNited imeichapa Polisi Mara, na kutinga 16 bora