Mchezo wa Ligi wa Azam unaofata ni dhidi ya Simba
Azam FC inashika nafasi ya tatu (3) kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 64 katika michezo 32 ya VPL ikiwa imebakiza michezo miwili kabla ya kumaliza msimu, na leo watapimana ubavu na Transit Camp ambayo nayo inayojiandaa na mchezo wa mtoano ('play off') wa kuwania nafasi ya kupanda ligi kuu.
Huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa wanalambamba Azam FC wanacheza, mchezo mwingine wa kijrafiki uliopita ulikuwa dhidi ya Pamba FC ambayo nayo inajiandaa na mchezo wa Play off ya kupanda Ligi Kuuu na Azam ilishinda mchezo huo kwa mabao 3-0, mara ya mwisho Azam kucheza mchezo wa mashindano ilikuwa June 26 mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Simba mchezo ambao walifungwa bao 1-0.
Michezo miwili ya Ligi kuu iliyobakiza Azam ni dhidi ya Simba utakao chezwa Julai 14 katika dimba la Azam Complex na watamaliza msimu ugenini katika dimba la Mabatini Pwani dhidi ya Ruvu shooting Julai 18, 2021.



