
Azam FC imetimiza dakika hizo katika mchezo wa jana usiku baada ya kuitungua Ndanda FC bao 1-0 lililofungwa na Yahya Mohamed dakika ya 87, ukiwa ni mchezo wake wa 10 katika mashindano mbalimbali ikiwemo ligi kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la Mapinduzi.
Mechi hizo ni zile za ligi ilizoichapa Tanzania Prisons (1-0), Simba (1-0), suluhu dhidi ya Mbeya City (0-0), moto ulikolea zaidi ilipotwaa taji la Mapinduzi Cup bila kuruhusu bao ikiipiga Zimamoto (1-0), suluhu ilipocheza na Jamhuri (0-0), ikazigonga Yanga (4-0), Taifa Jang’ombe (1-0) na Simba (1-0).
Mchezo pekee ambao Azam FC imecheza mwaka huu na kuruhusu wavu wake kuguswa ni ule wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), ilipoichapa Cosmopolitan mabao 3-1.
Azam FC vs Ndanda FC usiku wa jana
Mbali na mechi hizo za mashindano, Jumatano iliyopita Azam FC ilicheza na Mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki na kufanikiwa kuwabana vilivyo na kupelekea kumalizika kwa sare ya bila kufungana.