Jumanne , 27th Sep , 2016

Bilionea wa Urusi, Roman Abramovich, amesema atatoa fedha za kutosha kwa Antonio Conte, kufanya usajili wa safu ya ulinzi ya Chelsea ambayo imeonekana ni uchochoro katika mechi mbili zilizopita za ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich

Mmiliki huyo amesema bado anamuamini kocha wa Chelsea Antonio Conte, na anataka kumpa mazingira mazuri ya kuwekeza zaidi katika idara hiyo ya ulinzi kwenye dirisha la usajili mwezi Januari mwaka ujao.

Chelsea imepokea vichapo viwili mfululizo dhidi ya Liverpool akifungwa 2-1 na kichapo cha aibu kutoka kwa Arsenal cha 3-0 Jumamosi iliyopita.

Tangu kuumia kwa mlinzi mkongwe John Terry wiki mbili zilizopita, bado walinzi Branislav Ivanovic na Gary Cahill, wameonekana ni mzigo katika safu ya ulinzi.