Jumatano , 27th Apr , 2016

Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuweza kushiriki katika michezo mbalimbali ili kujijengea mafanikio ya kimichezo hapa nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Makoye Alex Nkenyenge

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge amesema, mafanikio ya kimichezo yanatokana na ushiriki katika michezo hivyo wananchi wanatakiwa kuwa na mazoea ya kushiriki michezo mbalimbali na pia kuwapa sapoti hata wale wanaoshiriki.

Nkenyenge amesema, ushiriki wa michezo pia unakuwa na mashindano mbalimbali hivyo jamii inatakuwa kuwa na mazoezi pia ya kimichezo ili kuweza kupata wanamichezo wengi hapa nchini ambao wataweza kuiwakilisha nchi katika michezo mbalimbali ndani na njue ya nchi.

Nkenyenge amesema, makampuni mnbalimbali pia wanatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuweza kushiriki katika michezo ili kujenga afya na uwezo wa akili pamoja na kuunganisha watu wa umri mbalimbali pamoja na madaraja mbalimbali ya kumaisha kujiona kuwa sawa.