Jumanne , 7th Dec , 2021

Je ulikuwa unafahamu Ijumaa na Jumamosi ilikuwa ni wikiendi katika Umoja wa Falme za Kiarabu?

Moja ya picha ya majengo Uarabuni

Umoja wa Falme za Kiarabu umetangaza utahamisha wikiendi kutoka siku ya Ijumaa na Jumamosi na kuwa Jumamosi na Jumapili ili kwenda sawa na soko la uchumi ulimwenguni.

Kuanzia January 1, wafanyakazi wote katika falme za kiarabu watafanya kazi siku 4 na nusu kuanzia jumatatu mpaka Alhamisi na Ijumaa watafanya kazi mwisho mchana.

Mabadiliko hayo yataisadia Umoja wa Falme za Kiarabu kuimarisha uchumi na soko la mafuta kwa kwenda sawa na nchi nyingine Duniani ambazo kazi hufanyika kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa.