
Lakini watoto hao wanapokua, wakafikisha umri wa miaka 18 na zaidi unaowalazimu kuondoka nyumbani kwa wazazi, wengine hugoma kuondoka kisa mali za wazazi wao. Wengine hata kama wakiondoka na kuanza kujitegemea, bado hung’ang’ania mali za wazazi wao jambo ambalo huleta mkanganyiko ndani ya familia.
Hawa hapa ni baadhi ya wachangiaji ambao wameeleza sababu zinazochangia vijana kung’ang’ania mali za wazazi wao kwenye mada ya kipindi cha funguka kinachoruka kupitia EATV na ukurasaa wake wa Facebook, ambapo mada hiyo imeuliza “Unafikiri ni kwanini kwenye baadhi ya familia vijana hukomalia mali za wazazi wao “.
Sheila Binti Chifu: unapo komalia mali za wazazi wetu sio kwamba sisi hatuna uwezo wakutafuta vyakutu hapana, unakuta baba yangu na mama yangu wameishi zaidi ya miaka 35 au 40 wana mali nyingi lakini baba anaenda kuchukua mwanamke mdogo mwenye rika sawa na mimi anataka kumiliki mali zile na kuzitawala kuliko mama yangu aliye chuma tangu mwanzo wakiwa na baba, na pia baba zetu wakisha pata wake wadogo wanasahau kabisa wake zao wakubwa.
Makopa Tz: @Makopa Kutoka Tegeta Mimi naona makundi ndiyo yanayo waharibu wanashauriana vibaya wakiona mwenzao kaachiwa mali basi na yeye ataacha kufanya kazi au ataacha kusoma akijua wazazi wangu wanamali baada na yeye afanye kazi au asome na yeye aweze kuwa na mali kama za wazazi wake, wanashauriana ujinga... Ndiyo maana sisi vijana hatuendelei.
Shaly Masawe: KUTOKA MOSHI#funguka. Vijana wa sasa hawapendi kujituma kwa sababu wanaona kwa wazazi kuna mali nyingi zinawapa kiburi hawataki kujituma.
Generous Queenllu: Nafikiri ni sawa kufatilia ila wasitegemee mali za wazazi wanatakiwa watafute zao kwa nguvu zao....Mali ya mzazi inachangamoto sana#from songea.
Onesmo George: from green city #funguka kwa upande wangu naona ni makuzi ambayo walezi wetu wametulea yani tumelelewa kutegemea sana kuliko kutafuta wenyewe ni sawasawa na mfumo wa elimu yetu.
Sababu kubwa iliyotajwa na wachangiaji wengi kuwa ni tatizo kwa vijana hadi kufikia hatua hiyo ni uzembe na kutojituma miongoni mwa vijana wengi pamoja na malezi ya wazazi kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo.