Jumatatu , 6th Jun , 2022

Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe na Afisa Utawala kutoka The Guardian Limited, Bi.Rehema Shedrack Songor kupitia kampeni ya Namthamini wamechangia boksi 50 za taulo za kike ambazo zitasaidia kuwaweka shuleni watoto wa kike 50 kwa mwaka mzima bila kukosa masomo.

Bi. Beatrice Bandawe (kushoto) akipokelewa taulo za kike na Rita Chuwalo (kulia)

Watangazaji wa kipindi cha Mama Mia cha East Africa Radio, Ritha Chuwalo na Yustam Sowoya wamepokea taulo za kike katika ofisi za EATV Mikocheni, Dar es salaaam.

''Tumeona tutoe msaada huu wa boksi 50 za taulo za kike  kwa ajili ya wasichana wanaosoma ili kuwawezesha wasishindwe kuhudhuria masomo kwa sababu utafiti unaonyesha kuwa, katika siku 28 wanafunzi wa kike wanakosa masomo siku 4 kwa sababu ya kuwa kwenye hedhi na kukosa vifaa salama vya kuwahifadhi'' - Bi. Beatrice Bandawe

Pia unaweza kuwasilisha mchango wako wa PEDI au fedha katika ofisi za East Africa Television na East Africa Radio, Mikocheni Dar es salaam