
Lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia hasa katika mawasiliano, huenda suala la umbali lisiwe tatizo tena katika mahusiano kwasababu wapenzi hupata nafasi kubwa ya kuwasiliana kila wakati wanaohitaji kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama Facebook, Whatsapp, Instagram, Imo na mingine mingi.
Wadau mbalimbali wametoa maoni yao kupitia kipindi cha funguka kinachoruka kupitia EATV na mada inayowekwa ukurasa wa Facebook wa East Africa Tv, ambapo mada hiyo imeuliza “Umbali baina ya wapenzi hudhoofisha mahusiano ya wapenzi, ndiyo au hapana na kwanini?” na haya hapa ni baadhi ya maoni yao.
Amanya Ahmed Neema Daudi: #FUNGUKA ndio mahusiano ya mbali yanadhoofisha mapenzi kwa sababu ni kweli mtapanga kuvumiliana lakini ukweli wanaume ni ngumu mno kuvumilia kuwa mbali na mpenzi wake hivo hali hiyo upelekea usariti na maumivu upande wa pili.
Twalib Mswadiku : Wa chato geita hapana kwenyeee hili swala umbalii hausiki chochotee hapo Mimi naona kama mtuuu anakupenda kwa dhati atakuvumilia katika shida na raha,tuchukulie walee wanaosafiri kikazi.
Abbas Jiriwa: Sio kudhoofisha tu bali umbali hunyausha mapenzi. Asilimia kubwa ya wafanyakazi mapenzi huisha kwa staili hii, we chukulia wewe umepangiwa kazi makambako halafu mkeo au mumeo yupo tandahimba Mtwara, unategemea kwa baridi ya makambako utaweza kuvumilia kweli mpaka upate likizo? Labda kama wewe ni malaika.
Mwanahamisi Msangi: Ni kweli! Ila kama mnapendana kwa dhati hakuna kitakachoharibika; ila ikitokea mmoja wapo asipokuwa muaminifu hapo hakuna mapenzi tena unaweza ukamvumilia kumbe mwenzako kesha pata mwingine.
Grace Braixon: Naitwa Grace Braixon kutoka Nipo south Africa NDIYO: hudhoofisha kwa sababu na sababu yake kuna kauli Moja inaitwa kukata tamaa MTU awezi kungoja ngoja mda wote mapenzi ya mbali ayana matamanio.
Wengi kati ya wachangiaji wa mjadala huo wametofautiana na mada kuwa kigezo cha umbali ni sababu ya mahusiano ya wapenzi kudhoofika, wakidai kuwa mawasiliano ndiyo kiungo muhimu kwa mahusiano ambayo hutenganishwa kwa umbali.