
Msaikolojia Justus August
Akizungumzia hilo kwenye show ya DADAZ ya East Africa TV Justus August amesema hivyo kwa sababu ni ngumu kwenye mahusiano kukutana na mtu aliyekamilika kwa asilimia mia.
"Avarage time ya watu wa kudumu kwenye mapenzi ni miaka miwili mpaka mitatu, ikipita zaidi ya hapo basi utakuwa na bahati sana, kama unabisha angalia mahusiano mengi yanavunjika baada ya muda gani japo wengine wapo lakini hawapendani"
"Kibaiolojia Wanaume tunaongozwa na tamaa yaani tunatamani sana na ndizo zina-take action kwetu, mwanamke yeye anaongozwa na hisia ambazo zinampanda mdogomdogo kama unamtaka kwa kutumia zawadi, ujumbe mzuri, surprise na vishawishi vingine" ameongeza Justus August
Pia amesema kwenye mahusiano mkianza kuongelea matatizo kuliko malengo ni dalili za kuvunjika na dalili zingine ni kama kutopewa kipaumbele na kupuuza yale uliyokuwa unafanya au unafanyiwa mwanzo.