Kajala na Paula kuja na kipindi cha Tv

Alhamisi , 10th Jun , 2021

Mwigizaji Kajala Masanja na Mwanae Paula wanatarajia kuja na kipindi cha Tv (Reality TV Show) yao itakayoitwa ‘Mom & Daughter, Like Twins’ na itakuwa ni mfululizo (series) wenye mkusanyiko wa matukio mbalimbali ya nyuma ya pazia katika shughuli zao za kila siku.

Picha ya pamoja Kajala na Mwanae Paula

Kajala na Paula wame-share habari hizi njema kupitia kurasa zao za instagram kwa ku-post cover za ujio huo huku wakiacha ujumbe unaosema; 'Mom & Daughter "like twins" lifestyle reality show coming soon on your tv'.

Bado hawajaweka wazi ni kituo gani cha Tv ambacho kitarusha Reality show yao ya ‘Mom & Daughter, Like Twins’