Jumatatu , 19th Jun , 2023

Meneja Rasilimali wa ITV, Bi. Hellen Elipokea amekabidhi taulo za kike katika ofisi za East Africa TV & East Africa Radio kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ITV kwa ajili ya kampeni ya Namthamini ambapo wamechangia taulo za kike jumla ya pakiti 1200.

Balozi wa kampeni ya Namthamini, Justine Kessy wa tatu kushoto akipokea taulo za kike kutoka kwa Meneja Rasilimali watu wa ITV, Bi. Hellen Elipokea wa katikati.

Kampeni hii ilianzishwa mwaka 2017, kwa lengo la kuchangisha taulo za kike kwa wanafunzi wenye uhitaji mashuleni. Na mwaka huu ina lengo la kuwafikiwa wanafunzi 10,000.