Ajifungua watoto 10 kwa siku moja

Jumatano , 9th Jun , 2021

Mama Gosiame Thamara Sithole mwenye miaka 37 kutoka nchini South Africa ameweka rekodi ya kipekee kwa kujifungua watoto kumi kwa siku moja katika Hospitali iliyopo Jijini Pretoria.

Picha ya Mama aliyejifungua watoto 10 kwa siku moja

Mama huyo amejifungua watoto saba wa kiume na watoto watatu wa kike ambapo alikuwa ana ujauzito wa miezi saba na siku saba, pia kipindi cha nyuma aliwahi kupata mapacha ambao kwa sasa wana miaka 6, hivyo kwa sasa ana jumla ya watoto 12.

Akizungumza baada ya kujifungua watoto hao Mama huyo amesema "Nimeshtushwa na ujauzito wangu ilikuwa ngumu mwanzoni nilikuwa mgonjwa na ilikuwa ngumu kwangu"

"Sioni maumivu tena, ninaomba Mungu anisaidie kujifungua watoto wangu wote katika hali nzuri pia mimi na watoto wangu tutoke hai, napenda kuwa radhi juu yake"

Kwa upande wa mume wake aliyefahamika kwa jina la Mr Tsotetsi amesema ana furaha sana, yupo na hisia hivyo hawezi kuzungumza sana kuhusu suala hilo.

Chanzo : Standard.co.uk , Instablo9ja, Timesnownews, Africa News.