Ijumaa , 13th Mar , 2020

Kumekuwa na stori ambayo inaendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu ugomvi wa video vixen Binti Kiziwi na msanii wa filamu Wastara Sajuki, juu ya kumgombania Z Anto.

Z Anto na Binti Kiziwi kwenye picha moja upande wa kushoto, kulia ni Wastara Sajuki

Taarifa hizo zimekuja baada ya Wastara Sajuki, kumtishia kumchana na viwembe endapo ataendelea kuwasiliana Z Anto mida ya usiku, kwa sababu anamjua vizuri kuliko anavyomjua yeye.

Sasa kupitia show ya eNewz ya East Africa TV, imepiga stori na Z Anto mwenyewe ambaye amenyoosha maelezo kuhusiana na ugomvi huo.

"Sitaki kuongea sana kuhusiana na hii ishu ila Wastara ni mtu mzima na ikifikia hatua kuongea kitu ambacho kipo serious sijui kuna nini, siwezi kuwa sawa kutokana na kinachoendelea mitandaoni na pengine watakuwa na hasira zao binafsi" amesema Z Anto.

Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma Z Anto aliwahi kuwa kwenye ndoa na Binti Kiziwi, kisha kuachana baada ya miaka mitatu.

Tazama Z Anto akifunguka yote hapa