Picha ya msanii Whozu na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
Taarifa hiyo imetolewa na akaunti ya BASATA inayoeleza kuhusu maamuzi hayo baada ya kufanya kikao chini ya ya uongozi wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mwana FA na Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt Kedmon Mapana ndani ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Whozu alipewa adhabu ya kifungo cha miezi 6 na faini ya Tsh Milioni 3 wakati Mbosso na Billnass walipewa adhabu ya kufungiwa miezi 3 na faini ya Tsh Milioni 3.