Jumatano , 16th Jul , 2014

Msanii wa kundi la Goodlyfe Douglas Mayanja Sseguya, aka Weasel ambaye ametimiza miaka 29 mwezi uliopita, amesema kuwa yeye si shabiki wa masuala ya siasa ila anakubaliana na ufanisi wa kazi za viongozi nchini humo.

msanii Weasel wa nchini Uganda

Katika mahojiano yaliyofanywa na msanii huyo ameelezea kuwa anamfagilia mno askari polisi wa kike nchini humo anayeitwa Judith Nabakooba kutokana na utendaji wake wa kazi.

Weasle amemwagia sifa askari polisi huyo ambaye ni msemaji wa polisi akimwelezea kuwa ni mtu mtaratibu na msema kweli asiye kuwa na makuu katika utendaji wake wa kazi.