Jumatatu , 19th Oct , 2015

Wasanii wa muziki kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaani UDSM All Stars, wamekazia mchango wao katika kuhamsisha amani kuelekea uchaguzi, sambamba na harakati hizo kukiwa na kazi yao ya pamoja ambayo inasimama kwa jina 'Tanzania Mpya'.

msanii wa muziki kutoka 'We Belong To Art' Eberhard Komba wa nchini Tanzania

Ujumbe huo muhimu kutoka kwa kundi hilo la wanasanaa wasomi wanaofahamika kama 'We Belong To Art' ambao wameamua kuungana kama muunganiko wa vijana wenye vipaji mbalimbali vyuoni, katika kipindi hiki ambacho zimebaki takriban siku 6 watanzania washiriki katika zoezi la kupiga katika uchaguzi mkuu wa taifa.