
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema kuwa na mahusiano na wanawake waliomzidi umri kwanza ni sunna kwa imani ya dini yake ya Kiislam, lakini pia wanawake wakubwa wanatulia kwenye mahusiano, tofauti na wasichana wadogo ambao wanakuwa wasumbufu.
"Cha kwanza ni sunna, cha pili watoto pasua kichwa, ukiwa na mtu ambaye amekuzidi umri anaweza kukuongoza, siyo unakuwa na mwanamke anajua kuendesha gari halafu hajui kupika wali, unakuwa na mtu ameshakuwa na uzoefu wa maisha, kwa hiyo anataka kutulia", alisema Dogo Janja
Pamoja na kauli hiyo Dogo Janja amekanusha tetesi za kuwa na mahuisano na Uwoya, huku akiwataka mashabiki wake kufuatilia zaidi kazi zake ambapo sasa ana kazi mpya ya Ngarenaro, na sio kufuatilia skendo zake.