VIDEO: "Singeli tupunguze matusi" - Man Fongo

Thursday , 18th May , 2017

Msanii  Man Fongo amewataka wasanii wenzake wa kisingeli nchini kupunguza ukali wa maneno katika tungo zao wanazozitumia kwenye kuimba kwa madai muziki huo ndiyo pekee wa asili uliyobakia katika kulitangaza taifa kwenye soko la kimataifa

Msanii  wa miondoko ya kisingeli Man Fongo

Man Fongo amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz cha EATV huku akisisitiza kuwa muziki huo unasikilizwa na watu wa rika lote hivyo ni vizuri kwa wasanii kutumia mafumbo sehemu zenye matusi ili mtu awe na kazi ya ziada ya kulifumbua neno hilo lilikuwa linamaanisha jambo gani.

"Tupunguze kidogo ukali wa maneno kwa sababu ukiweka ukali wa maneno zaidi inawafanya watu wanashindwa kutuelewa kutokana sasa hivi muziki wetu umeshakuwa mkubwa unaeleweka na wakina mama, watoto wadogo pamoja na watu wazima...Tunataka tupambane tuzidi kufika kimataifa zaidi, asiwe anatoka Man Fongo tu leo kaenda huku basi kesho tumsikie mwengine kama Shoromwamba au nani.. Wote tutoke tupige muziki wetu tukautangaze....Tutoe ule ukali wa maneno kidogo, nikisema ukali wa maneno nina maanisha tutoe yale matusi kwa maana ukiongea kwa moja kwa moja utakuwa ujafumba inabidi ufumbe uweke katika mafumbo kidogo mtu awe na kazi ya kulifumbua lile neno". Alisema Man Fongo