Billnas amefunguka hayo hayo kupitia eNewz ya EATV na kudai kwamba anatamani mwaka huu ndiyo angekuwa anamaliza chuo na kuanza kufanya muziki kwani kuchanganya kazi na masomo kumempotezea pesa nyingi kupitia wimbo wa 'Chafu pozi' ambao ulimpatia shows ambazo alilazimika kuzipiga chini na kujikita na masomo zaidi.
"Kufanya muziki na chuo nimepoteza pesa nyingi sana, watu wengine hawawezi kujua, nimeshakataa 'show' nyingi sana, nimeshaacha kwenda kwenye matamasha kibao...Vitu vingi sana vya kimuziki vilinipita na ndiyo ilikuwa 'time' yangu, kipindi cha 'Chafu pozi' inawika nilikuwa napata dili nyingi sana yaani hela ambayo najua kabisa hata nikimaliza chuo nisiweze kuitengeneza lakini masomo yalinibana zaidi". Alisema Billnass
Mtazame hapa chini akifunguka kwa undani zaidi