Alhamisi , 28th Mar , 2024

Mwanasheria wa mwanamuziki #Diddy Aaron Dyer amepinga vikali uvamizi uliofanywa na Idara ya Usalama wa Taifa Marekani dhidi ya mteja wake nyumbani kwake Los Angeles na Miami.

Picha ya Diddy

Taarifa aliyoitoa Mwanasheria huyo inasema upekuzi huo uliofanywa ni uviziaji ambao haujawahi kutokea pia ni kama Uwindaji/Utafutaji wa Wachawi kwenye tuhuma zisizo na msingi zinazotolewa katika kesi za madai

Pia ameongeza kueleza kuwa Diddy hana hatia na ataendelea kupigania kusafisha jina lake ambalo linachafuliwa.

Bonyeza hapa chini kwenye video kujua madai ya kesi anazotuhumiwa nazo Diddy