Ijumaa , 1st Apr , 2022

Harmonize ana-make headlines sana mitandaoni kuhusu maelezo yake kwenye Instagram akieleza hali ya mahusiano aliyokuwa nayo akimlenga aliyekuwa mpenzi wake Kajala.

Picha ya msanii Harmonize

Kwenye maelezo hayo Harmonize anatumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza, lakini kuna baadhi ya maneno ya kiingereza yamekuwa yakijirudia kuchapia akiandika kwenye Insta Story yake.

Haya ni baadhi ya maneno aliyochapia kupitia maelezo yake ni 'Don't gev up on me' badala ya 'Don't give up on me' pia 'Im sorry i known how i didi you wrong' badala ya 'Im sorry i know i did you wrong'.

Maneno mengine aliyochapia ni parson akimaanisha 'Person' reson badala ya reason na miss understand ikiwa ni misunderstand.