Jumatano , 23rd Sep , 2015

Aliyekuwa mwigizaji maarufu kutoka nchini Kenya, Nana Gichuru aliyepoteza maisha mchana wa jana katika ajali mbaya ya gari, amegusa nyoyo za wengi ikiwepo sehemu kubwa ya watu maarufu nchini Kenya.

Aliyekuwa mwigizaji maarufu kutoka nchini Kenya, marehemu Nana Gichuru

Watu hao wakiwemo wadau na mashabiki wake kwa njia ya mtandao wameendelea kuanika hisia zao za mshtuko na huzuni kufuatia tukio hilo.

Avril Nyambura, Brenda Wairimu, DNG na wengine wamekuwa ni kati ya mastaa ambao wameongelea kifo hicho, huku wakiguswa zaidi na maneno ambayo marehemu aliandika mwenyewe katika mtandao wiki mbili zilizopita, sehemu yake ikisomeka "Life's journey is not to arrive at the grave safely in a well preserved body, but rather to skid in sideways, totally worn out" maneno ambayo yanakuwa ni kama utabiri wa kifo chake.

Bado hakuna taarifa za mipango ya mazishi ya star huyo ambaye katika kipindi cha uhai wake alijishughulisha na uigizaji, uandishi, upigaji picha, muziki na mambo mengine mengi ya kisanaa.