
Alikiba na Killy
Ubishi huo ulikuja wakati wanatambulisha ngoma yao mpya ya Gubu katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, ambapo wote wawili walikuwa wanazungumzia uzoefu wao juu ya suala la kuumizwa katika mapenzi.
"Unajua kwenye maisha ya mahusiano kunakuwa na purukushani za hapa na pale zinatokea kila muda na kila wakati na hakuna ambaye hajawahi kukutana na misukosuko, kama sasa hivi tunaongea kuna wengine wanagombana huko, wanafukuzwa na kutolewa nguo nje anaambiwa atoke hatakiwi tena" alieleza Killy.
"Mimi sijaoa ila uzoefu wangu kwenye mapenzi kuhusu kuwa na mtu ishawahi kunitokea na nikaumia sana karibia siku 5 hata kula hauli na vingine ni siri yangu ila wacha wajue tu kama nimeshaumia" ameongeza.
Aidha kwa upande wa Alikiba alimpinga Killy na kusema huwezi ukaumizwa kwa siku tano katika mapenzi labda iwe mwezi kwa sababu hali hiyo inapotokea inakuwa kama mdhaliliko.
"Mimi kwenye uzoefu ambao nimeupata katika mapenzi kwanza ulivyoumia wewe ni tofauti ambavyo nitaumia mimi, kila mtu anaumia kimpango wake, na hayawezi kukuacha hivihivi maana hayaridhiki yatakushurutisha, muda mwingine unaweza kujidanganya upo fresh kumbe unaumia" amesema Alikiba.