Ijumaa , 30th Jun , 2017

Msanii wa filamu nchini na Rais mpya wa FM Academia, Patcho Mwamba amefunguka kwa kusema haoni tatizo kwa bendi za muziki kutumbuiza katika kumbi za baa kwa kiingilio cha vinywaji kwa kuwa wanachoangalia ni pesa wanazolipwa.

Pacho ameeleza hayo kwenye eNewz ya EATV baada ya kuwepo na dhana kwa kipindi kirefu kuwa bendi zikiwa zinatumbuiza ni kujishusha hadhi kwa kuwa kiingilio chake kinakuwa ni kidogo mno huku wengine huweka vinywaji kama kiingilio getini.

"Nakwambiaje bendi ni kama daladala, tunahitaji mtu yeyote apande haijalishi ni mwehu, jini, mchawi, kinachoangaliwa ni nauli yetu tu"alisema Patcho.

Pamoja na hayo, Patcho aliendelea kwa kusema "Tumetoka juzi kwenye mbio za mwenge hakukuwa na kiingilio tulilipwa chetu tukaenda kwenye kukimbiza mwenge, kampeni zikifika watu wanaendaga bila ya kulipia kiingilio. Brand haiwezi kuuliwa kwa masuala ya vinywaji ni upotofu, sisi tukishakodiwa na tukipewa pesa yetu tunaenda kupiga hata kama chooni tutapiga si tumeshalipwa" alisisitiza Patcho.

Mtazame hapa anavyofunguka zaidi.