Alhamisi , 15th Feb , 2018

Msanii wa filamu nchini Tanzania na Rais wa watoto, Tausi Mdegela amefunguka na kudai hawezi kuwa na mahusiano na mwanaume limbukeni wa kujionesha kwa watu kila kitu wanachokifanya wakiwa pamoja.

Tausi Mdegela.

Tausi amebainisha hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri wakati alipokuwa anajibu swali lililoulizwa na muongoza kipindi hicho kuwa huwa anaangalia vigezo gani pindi anapotaka kuwa na mwanaume.

"Napenda mwanaume awe 'natural' kuhusiana na rangi yake, awe mwembamba, ajitambue kama yeye ni mwanaume maana kuna wengine wanasifa sana mpaka wana kera, sipendi mwanaume mshamba, limbukeni", amesema Tausi.

Kwa upande mwingine, Tausi amedai hii ndio mara yake ya kwanza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii.

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.