Alhamisi , 17th Jun , 2021

Msimu wa 21 wa ugawaji wa tuzo za BET unatarajiwa kufanyika siku kumi zijazo (Juni 27) huku muigizaji Taraji Penda Henson akitangazwa kuwa ndiye mshehereshaji wa tuzo hizo wakati mwanamuziki na muigizaji Queen Latifah akitarajiwa kupewa tuzo ya Lifetime Achievement Award.

Picha ya muigizaji Taraji Henson

Mwezi Mei 27, 2021 waandaaji wa tuzo walitangaza vipengele na wasanii wanao wania huku Rapper DaBaby na Megan Thee Stallion wakitokezea kwenye vipengele 7 kila mmoja  mbele ya Cardi B na Drake walitokea kwenye vipengele 5.

Tuzo za BET huandaliwa kwa lengo la kusherehekea mafanikio katika nyanja mbalimbali katika kazi ya sanaa ikiwa ni pamoja na burudani (Entertainment), muziki, michezo na Sinema (Movie).