Jumatano , 20th Mar , 2024

Msanii wa vichekesho, Umar Iahbedi Issa maarufu ‘Mzee wa Mjegeje’ amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mchekeshaji Mzee wa Mjegeje

Meneja wa msanii huyo, Real Jimmy amethibitisha taarifa hizo.

Mzee wa Mjegeje alitrend mitandaoni na msemo wake wa “Mimi mwaka huu kama sijashika milioni 10, 12, laki 5 nashika bunduki, mjegeje baba nasema nao tu, za kichwa za kichwa”.

Zaidi tazama hapo chini kwenye video taarifa kamili ya kifo chake.