Jumapili , 25th Jan , 2015

Historia mpya kwa upande wa tasnia ya burudani imeandikwa siku ya leo ambapo tamasha kubwa la Tigo Kiboko Yao limefanyika na kuwaleta pamoja juu ya jukwaa moja wasanii 18 wanaofanya vizuri kabisa katika chati za muziki hapa Bongo.

Meneja Mkuu wa Tigo aliyemaliza muda wake Deigo Gutierrez (kushoto), akimkaribisha mrithi wa nafasi yake Bi. Cecile Tiano na Vilevile Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara kwaajili ya kuzindua rasmi huduma ya Tigo Music katika viwanja vya Leaders Club

Tamasha hili limeenda sambamba na uzinduzi wa huduma ya Tigo Music, tukio lililofanywa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara.

Huduma hii mpya inawawezesha wateja wa tigo kupata burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wanaowapenda ndani na nje ya Tanzania na kujitengenezea playlist ya muziki kupitia 'application' inayotambulika kwa jina la Deezer.

Tukio hili kubwa limepambwa na burudani ya bandikabandua kutoka Sikinde Band, Msondo Band, Christian Bella akiwa na Malaika Band, Isha Mashauzi na timu yake ya Mashauzi Classic, Yamoto Band ambao pia walipewa shavu jukwaani na Christian Bella kupafom live kolabo yao.

Mastaa waliong'arisha zaidi shoo zao ni pamoja na Jux aliyefanya ngoma zake kabla ya kupewa shavu jukwaani na Young Dee kupafomu live colabo yao ya Sio Mchoyo, Vanessa Mdee akimpandisha jukwaani Barnaba kuimba pamoja 'Siri' na vile vile Fid Q akilishambulia jukwaa kwa kushirikiana na Stamina, Young Killer na kumtambulisha kwa jukwaa rapa chipukizi anayekwenda kwa jina Kifa.

Katika onesho hili ambalo limeendeshwa vizuri na ma MC TBway 360, Kenedy The Remmedy, Mwanne, Sam Misago pamoja na Dullah Mjukuu wa Ambua, kati ya wasanii wengine waliopanda Jukwaani ni Weusi, AY, Mwana FA, Profesa Jay, Shaa, Ben Pol, Linah, Shilole, Khadija Khopa, kivutio cha kipekee pia kimekuwa ni maonesho ya wasanii Ali Kiba pamoja na Diamond Platinumz jukwaani.

Fid Q a.k.a Ngosha jukwaani