Jumanne , 4th Mar , 2014

Supastaa anayetikisa chati za muziki Afrika na sehemu mbali mbali duniani, Davido kutoka nchini Nigeria, ametangaza mpango wake mkubwa kabisa wa kuzindua albam yake ya Skelewu mwezi huu huko UK.

Hatua hii ya Davido kuupeleka uzinduzi wa albam yake hii huko UK, Umekuja kutokana na ukweli kuwa msanii huyu amefanikiwa kujitengenezea idadi kubwa ya mashabiki huko Ulaya, ambao wanaopenda muziki anaofanya.

Uzinduzi huu kwa mujibu wa Davido ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina Aye, utafanyika tarehe 17 mwezi Machi na taratibu zote za maandalizi mpaka sasa zinakwenda sawa.