Alhamisi , 29th Feb , 2024

Mwimbaji wa muziki wa Bongofleva Dogo Janja amewahi kusimulia safari ya maisha yake wakati anaanza muziki mkoani Arusha, katika tamasha lililoandaliwa na kampuni moja ya simu, ilikuwa Juni 25, 2018. Janjaro alisimulia;

‘Nakumbuka mwaka 2009, Berry Black alikuja Tripple A (Arusha) kwenye show akauliza mtoto anayeweza kuimba wimbo wake ajitokeze, nikajitokeza, nikaimba wimbo wake wa Mi Nataka Kuwa na Wee, nikaimba vizuri akanipa Shilingi Elfu 20, nikatoka na mtiti wa watu wengi hii barabara mpaka Ngarenaro’.

‘Wakaniuliza unataka nini, nikawaambia mi nataka simu, wakaniambia kwanini unataka simu ya dukani? Lete hiyo hela tukakuibie simu tukuletee, huwezi amini simu yangu ya kwanza ilikuwa ya wizi, Mungu anisamehe’ – Dogo Janja