Jumanne , 17th Nov , 2015

Msanii Nuhu Mziwanda amesema katika maisha yake hajawahi kufikiria kufanya kazi nyingine zaidi ya muziki, kwani ndiyo ilikuwa ndoto yake.

Nuhu Mziwanda ameyasema hayo katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kueleza kuwa ilifikia hatua aligombana na mama yake mzazi kwa kuwa alikuwa anapenda sana muziki.

“Hiyo dream sinaga akilini mwangu, kwa sababu mi nakumbuka tangu nipo primary, ujue mtu unaanzaga kujitambua la kwanza la pili, kuanzia la pili la tatu nimeanza kupenda muziki, na muziki wenyewe nimeanza kupenda kupiga ngoma shuleni, kwa hiyo nilikuwa sifikiriagi akilini mwangu mi naweza kuwa rubani, mi nilikuwa napenda tu muziki hadi nilikuwa nagombana na bi mkubwa kwa sababu nilikuwa napenda muziki”, alisema Nuhu Mziwanda.

Nuhu aliendelea kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa ametimiza ndoto yake mpaka kuwa producer, na ana malengo ya kuwa mfanyabiashara kwa kuweka vitega uchumi mbalimbali.

“Nashukuru Mungu dream yangu ambayo nimeanza nayo tangu niko mdogo hadi leo bado naendelea nayo, kikubwa kingine nitaweka biashara na vitega uchumi vingine vikubwa ambavyo vinaweza ku run maisha yangu ukiachana na muziki, lakini nataka maisha yangu yaendeshwe na muziki”, alisema Nuhu.