
eNewz ilimtafuta Q Boy ili kujibu mitazamo hiyo na kusema si kweli kuwa Rayvanny na Shetta wametumika kumbeba kwenye ngoma hiyo.
“Mimi sijamuomba Shetta wala Rayvanny waingize sauti kwenye ngoma hiyo, wao wenyewe ndiyo walitaka kuingiza sauti zao na hata kabla ya wao bado ngoma ilikuwa kali”
Pia aliongeza kwa kusema kuwa kabla ya kutoa wimbo pia huwa wanamshirikisha Diamond ausikilize kwanza kabla haujatoka ili kama kuna kitu cha kuongeza aongeze.