Katika kipengele hicho, Shusho anachuana na wasanii wengine wakali kutoka Afrika Mashariki, Coopy Bly, Exodus, Father Micheal na Wilson Bugembe kutoka Uganda, Gaby Kamanzi wa Rwanda, na Rebecca Soki wa Congo.
Kwa sasa zoezi la kuwapigia kura washiriki kuwawezesha kushinda linaendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja, kwa njia mbalimbali ikiwepo mtandao, kuelekea zoezi kubwa ugawaji wa tuzo hizo kwa washindi June mosi mwaka huu.