Kwa mwaka huu, onesho hili linatarajia kuwaleta pamoja wabunifu mavazi 24 tofauti kuonesha kazi zao za ubunifu kwa siku 3 mfululizo.
Onesho hilo pia linatoa nafasi wa wabunifu wanaochipukia kupata jukwaa la kuonesha vipaji vyao ambapo kutakuwa na shindano la kuwapambanisha uwezo wao.