Jumapili , 29th Nov , 2015

Nyota wa muziki wa miondoko ya bongofleva mwenye makazi yake nchini Sweden Sara Larsson maarufu kama Saraha amepata shavu kushiriki katika tamasha kubwa la muziki lililobatizwa jina la Melodifestivalen 2016.

Nyota wa muziki wa miondoko ya bongofleva mwenye makazi yake nchini Sweden, Saraha

Saraha ameiambia enewz kuwa katika mashindano hayo makubwa mshindi ataiwakilisha Sweden katika Mashindano Makubwa ya nyimbo kwa nchi za Ulaya, zijulikanazo kama "Eurovision Song Contest", mashindano ambayo yameanza tangu mwaka 1956.

SaRaha ataimba wimbo maarufu wa mchanganyiko wa kiafrika, "Afro Pop" kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili, hii itakuwa nafasi kubwa kwa SaRaha kuutambulisha muziki wenye vionjo vya Kiafrika, yaani "Afro Pop" kupitia lugha ya Kiswahili kwa wapenzi wa Muziki wa Ulaya, kwani mwanamuziki anaeshiriki mashindano haya anapata nafasi kubwa ya kuutangaza muziki wake.

Mashindano haya yataanza mwanzo wa mwezi February na kuisha mwezi May 2016.