Quick Rocka ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa kupitia sanaa hiyo vijana wengi watajiajiri hivyo kuchangia ukuzaji wa pato la taifa.
"For instance muziki au sanaa kwa ujumla ni kitu ambacho serikali ikiwekea mkazo kwamba tunafanya kazi kuna kulipa kodi, itaingiza pato kubwa sana na kukuza uchumi wa nchi kama ikichukuliwa serious, coz vijana wengi wamejiajiri kupitia sanaa za maigizo, muziki, uchongaji na uchoraji, ni vitu ambavyo watu wanapenda kufanya", alisema Quick Rocka.
Pia Quick Rocka amesema viongozi na jamii inatakiwa ijue kuwa vijana ndiyo taifa la leo na nguvu kazi ya taifa, hivyo iwapo watatilia maanani yale wanayoyafanya yatakuza uchumi.
" Viongozi na watu wengine wote inabidi wajue kwamba vijana ndiyo taifa la leo, sisi ndiyo nguvu kazi ya taifa, kwa hiyo waki-concetrate kwa vitu gani vijana wanapenda kujishughulisha navyo, maana yake ni rahisi zaidi uchumi kukua na vitu vingine", alisema Quick Rocka.