Jumatano , 12th Mei , 2021

Rapper Salmin Swaggz ame-sign dili na Apple Music kupitia kampuni ya 'Platoon' ambayo husaidia wasanii huru kufadhili, kusambaza na kuuza kazi zao za muziki.

Msanii Salmin Swaggz

Hii ni kama lebo huru ya muziki iliyokusudia kuwanyanyua wasanii barani Afrika kimasoko katika biashara ya muziki na imefanya kazi na wasanii wakubwa kama Billie Eilish, Stefflon Don na wengine wengi. 

“Don't Act Like You Know Me ni wimbo wangu wa kwanza kuachia chini ya Platoon, humo amesikika Country Boy kwenye chorus ingawa haikuwa kama collabo kwasababu za kimkataba na lebo yake, ila kwasababu video sija-shoot nafikiria  ahusike kwenye verse moja ili ilete maana nzuri” – amesema Salmin.

Wimbo huo ulirekodiwa mwaka 2019 na Paul Maker wakati yupo Roof Top huku mixing na mastering ikifanyika mwaka huu na Lufa.