Jumatatu , 4th Sep , 2017

Msanii wa muziki Tanzania mwanamama ambaye ana sauti yenye mvuto wa kipekee Saida Karoli, amewavuta wasanii wawili wa bongo fleva, G Nako na Belle 9, kwenye kazi yake mpya ya 'Kichaka'.

Saida Karoli

Kazi hiyo ambayo imeachiwa jana video yake imefanywa na Hanscana, imeonyesha kuzidi kumuweka pazuri Saida Karoli, kutokana na ubora wa video uliopo, na jinsi wasanii hao walivyoweza kuibeba nyimbo hiyo.

Kwenye wimbo huo rapper G Nako kutoka Weusi ameonekana akiimba na kuchana, kitu ambacho anakimudu vema.

Itazame hapa chini