Jumapili , 3rd Jan , 2016

Meneja wa kituo cha Wanawe na diwani wa Kata ya Kirungule Said Fella amesema kuwa mwaka 2016 unaonyesha utakuwa ni wenye mafanikio makubwa kwa wasanii kutoka tasnia mbalimbali za burudani nchini.

Meneja wa kituo cha Wanawe na diwani ya Kata ya Kirungule Said Fella

Mkubwa Fella ameongea na enewz kuwa kinachopaswa kufanyika kwa wasanii ni kujitengenezea wigo mkubwa kupitia kazi zao, na pia kuacha kulaumiana bali wajitengenezee njia za kupata maslahi yao kupitia vipaji vyao.

Aidha Fella amesema amefarijika kuona kazi nzima ya kikundi chake kipya cha vijana wa kundi la Salamu TMK ambao hivi sasa video ya kazi yao mpya inayoitwa 'Nafsi' ikifanya vizuri kupitia stesheni mbalimbali za tv nchini.