Jumanne , 20th Oct , 2015

Said Fella au Mkubwa na Wanawe ambaye hivi sasa anawania nafasi ya udiwani kupitia kata ya Kilungule jijini Dar es Salaam amezidi kuwekeza nguvu zake katika kuinua zaidi vipaji ambapo hivi sasa amelivumbua kundi la vijana chipukizi linaloitwa 'Sallam

Kundi jipya la muziki la 'Sallam TMK' lililovumbuliwa na meneja Said Fella almaarufu kama Mkubwa na wanawe

Said Fella ambaye ameweka makazi yake katika kata hiyo ya Kilungule ameongea na eNewz kuwa ameona vipaji vya vijana wa jinsia mbalimbali ambao wana uwezo mkubwa katika sanaa ya muziki, ambao wanataka kusaidiwa kufikia kilele cha mafanikio yao katika sanaa hiyo.

Aidha Fella pia amegusia kuhusu mipangilio endelevu ya vijana wake wa 'Mkubwa na Wanawe' wa Yamoto Band pamoja na bendi mpya ya Moyo Modern Taarabu.