Jumapili , 9th Mar , 2014

Unaweza jiuliza iwapo rapa Roma amekuwa mchungaji wa kondoo wa bwana kwa kuangalia picha alizozipiga lakini taarifa ni kwamba rapa huyu anatarajia kutoa wimbo wake mpya alioubatiza jina KKK ambao utatoka rasmi kesho yaani jumatatu.

Roma ameongea na eNewz akisema kuwa wimbo huo uliofayiwa kazi kupitia Tongwe Records ni wimbo ambao unaufungua mwaka 2014 kwa kishindo kwani baada ya traki hii kuna maandalizi mengine yatafuatia.

Aidha, mkali huyo ameweka wazi kuwa pamoja na picha ya cover ya Cd hiyo kuonyesha kwamba anawachunga kondoo haimaanishi kuwa ameamua kuwa mchungaji bali ni ubunifu tu alioamua kuutumia katika sanaa.