Ijumaa , 9th Aug , 2024

Kwenye mahojiano yake na kipindi cha PlanetBongo ya EastAfricaRadio, mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya Mazuu Record

..amefunguka kwa mara ya kwanza kwamba Rich Mavoko kwenda WCB siyo kwamba ni yeye alitaka bali alipitia kipindi ambacho ilihitaji kuchukua maamuzi ya kujiunga na label hiyo.

 

''Siyo kwamba Rich Mavoko ndiyo alitaka kwenda WCB ni wao ndiyo walitaka yeye aende kwao, kwa sababu alikuwa ni mtoto msumbufu kuliko Kiba, Rich Mavoko ni msanii pekee ambaye anaweza kuimba kwenye namna yoyote unayoitaka wewe'' - Mazuurecord akizungumza na PlanetBongo ya EastAfricaRadio