Jumatano , 5th Aug , 2015

Staa wa muziki wa Bongofleva Real Jofu ambaye ametoa video yake mpya iliyobatizwa jina “Kumbe Ni Ndugu” aliyomshirikisha mwanadada Ney Lee, ameiambia eNewz kuwa awali alipanga kufanya wimbo huo na staa Linah Sanga.

Staa wa muziki wa Bongofleva Real Jofu

Real Jofu ameelezea kuwa licha ya menejimenti yake Linah kutoweza kupata ruhusa hiyo, alianza mchakato wake wa kutafuta wasanii wengine wa kike ambao nao ilikuwa vigumu kwa staa huyo kuweza kuwapata wakiwemo Recho na pia Meninah ambao nao walikuwa na shughuli zao binafsi.

Real afunguka zaidi kuhusiana na mchakato huo wa kuwapata madiva hao hadi kufikia hatua ya kumnasa Ney Lee kuweza kushiriki katika video hiyo mpya.